Login for faster access to the best deals. Click here if you don't have an account.

Project Agronomist Full-time Job

Apr 23rd, 2022 at 14:51   Other   Sumbawanga   107 views Reference: 32
Job Details

Chama cha Ushirika cha Akiba Na Mikopo Mpui (MPUI SACCOS LIMITED) Chenye Usajili Namba RKR 358 ambacho kilianzishwa mwaka 2003 na kupata usajili rasmi Tarehe. 31.05.2004 chini ya Sheria ya Vyama Vya Ushirika- Tanzania.

Ushirika wa Mpui unajumuisha wanachama wakulima ambao ulima mazao kama Mahindi, Maharage na Alizeti na mazao mengine. Kuanzia mwaka 2016 hadi sasa Ushirika wa Mpui umejikita katika shughuli za kilimo kama;-

i. Kutoa Mafunzo ya Ugani,

ii. Mafunzo ya usimamizi wa uvunaji na uhifadhi salama,

iii. Utafutaji wa Masoko na Pembejeo

iv. Ukusanyaji wa mazao na menginyo.

Chama kimekuwa kinafanya kazi na wadau mbalimbali walio kwenye mnyororo wa kilimo kama Taasisi za Kifedha (MFI/FI), Taasisi zisizo za kiserikali (NGOs), Kampuni za pembejo (inputs’ companies), mashirika ya kimataifa ya maendeleo (International Development Agencies), Wafadhili wa miradi (Donors), wanunuzi wa mazao (Off-takers), Taasisi za utafiti, Taasisi za serikali na sekari za mitaa (LGA) na Serikali kuu (GA).

Tarehe 15 April 2022 Ushirika wa Mpui umeshinda RUZUKU kutoka Taasisi ya kimarekani ijulikanayo “UNITED STATES AFRICAN DEVELOPMENT FOUNDATION (USADF)”, ambayo RUZUKU hiyo itajikita kwenye mnyororo wa thamani wa zao la mahindi yaani.

Jina la Mradi ni Kuimarisha Uzalishaji wa Mahindi ya Mpui na Miundombinu ya Masoko’ – ‘’Strengthening Mpui Maize Production and Marketing Infrastructure’.

Lengo la Mradi; Kuboresha hali ya maisha na ustawi wa kiuchumi wa wanachama wa Mpui Wilayani Sumbawanga’

Muda wa Mradi: kuanzia Tarehe 15.04.2022 hadi 31.03.2025.

Hivyo basi Chama cha Akiba na Mikopo cha Mpui kinacho jumuisha wakulima wa zao la mahindi kutoka Taarafa ya Mpui kinatangaza nafasi ya kazi kama ifuatavyo:-

A. NAFASI YA AFISA KILIMO WA MRADI- USADF

Kituo cha Kazi

Ofisi za MPUI SACCOS LTD zilizopo Kijiji cha Mpui A karibu na Ofisi za mtendaji wa Kijiji cha Mpui A.

Idara

Kitengo cha kilimo, pembejeo na Masoko.

Kipindi cha kazi

Mkataba wa kazi unaweza kurejeshwa/rewa kulingana na utendaji wa kazi na upatikanaji wa raslimali fedha kutoka kwa mfadhili

Mshahara

Mshahara mzuri utatolewa lakini kwa njia ya majadiliano (with negotiation) kulingana na kiwango cha mfadhili kilichopo kwenye Bajeti

Lugha ya mawasilino

Kiingereza (English) wakati wa mazungumzo/vikao na wafadhili na kuanda taarifa za mradi.

Kwiswahili wakato wa mafunzo kwa wakulima na wadau wengineyo na wakati wa uwasilishaji wa taarifa zinapo hitajika na Bodi ya Uongozi ya MPUI SACCOS LTD

Kuwajibika kwa

Meneja Mradi (Project Manager)

Kusudi la Kazi

Msimamizi Mkuu wa masula ya uzalishaji wa mazao shamabani kwa wakulima.

Majukumu na majukumu muhimu:

· Kutoa mafunzo ya kanuni za kilimo boa cha mahindi na kutoa huduma za ugani,

· Kusimamia shughuli zote za kilimo- kuanzia uzalishaji hadi mavuno na utunzaji,

· Kuhamasisha wakulima wapya kujiunga na MPUI SACCOS/AMCOS LTD na kuingizwa kwenye utaratibu wa mradi

· Kuandaa taarifa za uzalishaji kwa ajili ya chama na wadau wengine wataohitaji,

· Kutoa mafunzo na kusimamia waliopata mafunzo ambao watafanya kazi kwenye vikundi chini yake,

· Kuhamasisha wakulima kujiunga na mradi

· Kwa kushirikiana na Meneja/kamati ya masoko/Bodi katika utafutaji wa masoko

· Kusimamia vikundi vya vijana katika uzalishaji

· Kuandaa na kutoa mafunzo kwa wakulima viongozi (ToTs)

· Kuandaa mpango kazi kwa kushirikiana na Meneja Mradi

· Kushiriki katika mafunzo ya mradi, tathimini ya mradi, na matembezi ya wafadhili au wadau wengineyo

· Kuunganisha wakulima na upatikanaji wa pembejeo.

· Atafanya kazi katika vijiji mbalimbali ambapo kuna wanachama wa MPUI SACCOS/AMCOS LTD walioko kwenye mradi

· Kusimamia mashamba darasa, Afisa kilimo mwanafunzi na wakulima kiongozi (ToTs)

· Atatoa taarifa mbalimbali za mapokeo kwa Meneja Mrado na kwa wafadhili wa mradi watakapo hitaji

· Kuaandaa taarifa kwa kushirikiana na Meneja/Mhasibu ya Robo Mwaka

· Atafanya shughuli zingine atakazo pangiwa na Meneja Mradi/Bodi.

Sifa za Afisa Kilimo Mradi Mradi Anayehitajika

· Awe na uzoefu wa muda usiopungua miaka miwili na kuendelea kwenye kufanya kazi kwenye mnyororo wa thamani wa zao la mahindi na mashirika kama; AMCOS/FBOs/CBOs/NGOs/INGOs/MFI/FI/SMEs N.K

· Awe na elimu isiyopungua Shahada/Astashahada ya Uhasibu

· Awe na umri usiopungua miaka 25 na usiozidi miaka 45

· Awe Mtanzania

· Awe na uwezo wa kufanya kazi katika usimamizi duni

· Awe na ujuzi wa kutumia vyema Kompyuta na Programming zake kama vile Microsoft office package kama EXCEL,, word, power point presentation, SPSS 16.0, KENGA Moible, MIS Database system

· Uelewa mkubwa juu ya kilimo cha mahindi na kilimo himilivu kinachoendana na mabadiliko ya tabia ya nchi

Uwezo muhimu

· Mwajibikaji na mmakini kwa maelezo (Accountability and attention to details

· Mtafakari kwa kina (Analytical and critical thinking)

· Muadilifu (Intergrity)

· Uwezo wa kufanya kazi kwa pamoja na ushirikiano (Team work and cooperation)

· Ni mjuzi na mbunifu

· Mwenye uwezo wa kuandaa taarifa mbalimbali

Vigezo vya kuchagua/ kumpata mhasibu wa mradi (Selection criteria)

· Ustadi wa kuzungumza na kuandika katika Kiingereza na Kiswahili

Malipo (Remuneration)

· Mshahara Mzuri kwa Mwaka utatolewa kwa ushindani na faida nyinginezo kitatolewa kama NSSF, WCF, Mawasiliano, Internet, Usafiri wa ndani na Nje (Free Local/International trave).

Viambatanisho

· Barua ya Muombaji

· Wasifu wa muombaji usiozidi kurasa tano

· Nakala za vyeti vya kuhitimu na nakala nyinginezo

· Cheti cha kuzaliwa

· Nakala ya kitambulisho cha Taifa/ Namba ya kitambulisho (NIDA)

Muda wa kutuma maombi

Kuanzia Tarehe 16.04.2022 hadi 25.04.2022.

Aina ya kazi (Job type)

Kazi ya kudumu wakati wa mradi.

Mahali pakazi

Mpui, Wilaya ya Sumbawanga vijijni.

Jinsi ya Kutuma Maombi (How to Apply)

Maombi yote ya kazi yatumwe kwa njia ya barua pepe [email protected]

Maombi yaelekezwe kwa ‘MWENYEKITI WA BODI’

Kwa kuijua zaidi MPUI SACCOS/AMCOS tembelea

Website yetu: www.mpuiamcos.co.tz

Mawasilisho yaliyowasilishwa kwa mikono na mawasilisho yaliyo cheleweshwa hayatazingatiwa.

Company Description
Chama cha Ushirika cha Akiba Na Mikopo Mpui (MPUI SACCOS LIMITED) Chenye Usajili Namba RKR 358 ambacho kilianzishwa mwaka 2003 na kupata usajili rasmi Tarehe. 31.05.2004 chini ya Sheria ya Vyama Vya Ushirika- Tanzania. Ushirika wa Mpui unajumuisha wanachama wakulima ambao ulima mazao kama Mahindi, Maharage na Alizeti na mazao mengine. Kuanzia mwaka 2016 hadi sasa Ushirika wa Mpui umejikita katika shughuli za kilimo kama;-i. Kutoa Mafunzo ya Ugani, ii. Mafunzo ya usimamizi wa uvunaji na uhifadhi salama, iii. Utafutaji wa Masoko na Pembejeo iv. Ukusanyaji wa mazao na menginyo.